BONYAD AKHTAR TABAN
Majlisi ya kuomboleza msiba ya aba abdilah al-Hussein na unuwani ya haiyya alaalaza
kwa kuingia kumi la kwanza la mwezi wa muharam pamoja nakuchukuwa tahadhari ya kuenea kwa ugonjwa wa corona na kukatazwa mikusanyiko. bonyad Akhtar taban waliamua kuanzisha majlisi ya aba abdillah al-huusein kwa jina la haiyya ala al azaa katika mitandao ya kijamii .
Majilisi hizi zilifanyika kwa lugha za Kingereza ,kiswahili,kiurudu ,kigijirati na kurushwa katika mitandao ambazo ni khutba na kaswida za kubainisha fadhila,ubora na mateso ya watu wa nyumba ya mtume .
Na kwa kulingana na udogo wa sehemu kijiografia Na kuwa na wasikilizaji tofauti tofauti majlisi hizi zilifanyika kwa masaa tofauti ya siku na kuwekwa kwenye chaneli ya YouTube na ambayo ilipendwa na wapienzi wa abba abdillah.