BONYAD AKHTAR TABAN

Kikao cha wawakilishi wa nchi za Africa mashariki

wawakilishi waheshimiwa wa nchi za africa mashariki walialikwa na bonyad Akhtar taban kwa kikao katika ukumbi  wa mikutano na kikao hicho kilifanyika chini ya usmamizi wa msimamizi wa ndani wa bonyad na msimizi wa utafiti wa bonyad.
kikao hicho kilifanyika kwa kuhudhuriwa na wawakilishi wa nchi za Tanzania Kenya,Uganda,Ruwanda,congo. kila mmoja wawakilishi waheshimiwa  waliongelea kuhusu  kazi za Allamah Sayyid Rizvi katika Africa mashariki na athari za shughuli hizo katika kuwaingiza watu katika dini ya kiislamu na madhehebu ya kishia na athari zilizobakia za Allamah Rizvi katika sehemu hizo na walishukuru pamoja na kutaja ukumbusho wao pamoja na allamah Akhtar Rizvi.
Kiongozi wa ndani aliongelea shughuli za kabla na malengo ya baadae ya muda mfupi na muda mrefu ya bonyad Akhtar taban.
Na katika kuendelea alizungumzia hali ya waislamu makhususi masheikh wa Africa mashariki ambapo kila mmoja wa wakilishi hawa walizungumzia hali ya sehemu walizotokea na waliwaomba waliohudhuria kutafuta njia ya kutatua matatizo yao khasa matatizo ya masheikh na kama katika waliohudhuria wana njia ya kutatua matatizo hayo waibainishe ili iweze kuwasaidia katika kutatua matatizo hayo .
Na mwishoni mwa mkutano huu waliohudhuria walielezea jinsi gani walivyoingia katika dini ya kiislamu na madhehebu ya kishia  pamoja na kuwa katika familia zao kuna madhehebu tofauti na jinsi ya kuamiliana nao pamoja na tofauti zao.
Itakumbukwa kuwa katika Africa mashariki kuna madhehebu tofauti tofauti lakini wanaishi kwa amani na utulivu  tofauti na maeneo jirani ambao sio hivyo ambayo ni mazingira mazuri ya kufanyia shughuli tofauti tofauti.
Mkutano huo ulimalizika kwa kumsomea suratu al-fatiha kwa ajilia marehemu allamah Rizvi  na kumswalia mtume (s.w)

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button
×