BONYAD AKHTAR TABAN
Hafla na mazazi ya Imam Jawad (a.s) ilifanyika pamoja babu yake mtukufu jirani na Haram tukufu ya dada yake Imam Ridhwa (a.s) katika mji wa Qom
Kusoma Mashairi na Tawasul zilikuwa ndio ratiba muhimu za Kikao hiki.
Katika kikao hiki ambacho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Buniyad Akhtar Taban yalitolewa Mashairi kwa Lugha ya Kiurdu kuhusu Ukarimu na Utukufu na Sira ya Imam Jawad (a.s) na Imam ali (a.s).
Katika kikao hiki walihudhuria wageni mbalimbali kutoka Mataifa tofauti India,Pakistan,Iran na Mataifa ya afrika Mashariki.
Kikao hiki kilianza baada tu ya swala ya Magharib na Ishaa kwa Kisomo cha aya za Qur’an Tukufu na kilimalizika kwa Kumsifu na kutawasali kwa Imam Ali (a.s).
Na kwenye tamati ya kikao hiki mjukuu wa Marhum Allamah Rizvi (r.a) Hujjatul-Islam wal Muslimin Sayyid Kadhim alionana na Waalimu wa Hawza na Vyuo vikuu.