Buniyad Akhtar Tabani yaandaa futari katika ofisi yake Futari hiyo ilihudhuriwa na Ayatullah Sayyid Mundhir Hakim na Sheikh Abdul-Muhsin Al-Baqshi Raisi wa hawza ya Alul-Bayty
Wageni rasimi wa kikao hiki walikuwa ni Raisi wa hawza ya Alul-Bayt (a.s) na Ayatullah Sayyid Mundhir Hakim. Wageni wengine katika kikao hiki walikuwa ni kutoka Mataifa ya Afrika Mashariki.
kikao hiki kilianza kwa Swala ilioongozwa na Ayatullah Sayyid Mundhir Hakim na kwenye muendelezo wa kikao hiki baada ya futari, waliohudhuria walielezea maoni yao kuhusu Marhum Allamah Sayyid Saed Akhtar Rizvi (r.a) na shughuli za Bonyad Akhtar Taban na walionesha Matarajio yao Juu ya Taasisi hii, Njia ambayo Marhum Allamah Rizvi aliianzisha ndio njia ile ile ambayo Babu zake walio wema waliianzisha na sasa hivi Mjukuu wa Allamah, Hujjatul-Islam wal Muslimin Syed Kazim Rizvi anaendeleza njia hii, na njia hii kamwe haitobaki pweke.
Mazungumzo ya wageni yalifika tamati kwa Ufafanuzi wa Ayatullah Sayyid Mundhir Hakim ambapo alitafsiri Suratul-Kauthar na sababu za kushuka Sura hiyo na Misdaq (mfano) wa Sura hiyo ni Watoto wa Bibi Zahraa (a.s).
Mwishoni mwa kikao hiki Maustadhi wote waliohudhuria katika kikao hiki walipewa zawadi na Hujjatul-Islam wal Muslimin Seyd Kazim Rizvi, zawadi hiyo ilikuwa ni Ubao wenye kipande cha Zulia ya Imam Ridhwa (a.s).