Habarinyumba ya sanaa ya picha

Biography Fupi ya Dokta Kanju

Imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za Kifo cha Dokta Mohammed Saleh Kanju, kilichotokea leo hii (17-06-2023) katika Hospital ya Mloganzira, Jijini Dar-es-Salam, Tanzania.

Dokta Kanju alikuwa ni Mubaligh madhubuti aliyeyatumikia vizuri Maisha yake katika kuyahudumia Madhehebu ya Ahlul-Bayt (as) katika kusambaza Mafunzo na Maarifa sahihi ya Uislamu Asili wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w).

Na huo ndio Mwisho Mwema wa mja Mwema wa Allah(swt) – kama alivyosema (swt):

“Na Mwisho mwema ni wa wale Wamchao Mwenyezi Mungu”.

🔻
Biography Fupi ya Dokta Kanju:

Dokta Kanju alikuwa karibu sana na Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi(ra) katika kazi za Tabligh, na kazi kubwa aliyokuwa akiifanya sambamba na Allamah S.S.A.Rizvi (ra) ni kutafsiri (Kutarjumu) elimu na maarifa mbalimbali ambayo Allamah Sayyid S.A.Rizvi(r.a) alikuwa akiyaandika kwa lugha ya Kiingereza, yeye alikuwa akifanya kazi ya kuyaweka maarifa hayo katika Lugha ya Kiswahili.

Kwa wasomi wa vitabu vya Allamah Rizvi (ra) na waandishi wengine kwa lugha Kiingereza, wanamtambua zaidi Dokta Mohammed .S.Kanju kupitia kalamu yake, kwa sababu kalamu yake imetumika kwa asilimia 99% kusambaza ilmu na maarifa ya Ahlul-Bayt (as) kwa kutafsiri vitabu hivyo kutoka lugha ya Kiingereza kwenda katika lugha ya Kiswahili, kiasi kwamba wafuasi walio wengi wa Ahlul-Bayt (as) wamenufaika zaidi na vitabu hivyo na wengine kubahatika kushikamana na Madhehebu ya Haki baada ya kupata Maarifa ya kutosha kupitia vitabu hivyo.

🔻
Ifuatavyo ni listi fupi ya baadhi ya vitabu vya Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi(ra) – na baadhi ya waadishi wengine – kwa Lugha ya Kiingereza, ambavyo Marhumu Dokta Mohammed S.Kanju alivitarjumu kutoka lugha ya Kiingereza na kuviweka katika Lugha ya Kiswahili:

1-Isma ya Mtume (saww) katika Qur’an 2- Fadak 3-Fitna za Mawahhabi Zafuchuliwa 4-Hijabu (Mavazi ya Unyenyekevu katika Uislamu) 5-Imam Al-Mahdi (atfs). 6-Imamate (Makamu wa Mtume s.a.w.w). 7-Maana na Chanzo cha Ushia. 8-Salman Farsi (Salman Mfursi) Rafiki wa Mtume Muhammad (s.a.w.w). 9-Siku ya Kiyama. 10-Taqiyya. 11-Usafi wa Mwili na Utakaso wa Roho. 12-Utetezi wa Sheria za Kiislamu (Muhtasari nne juu ya Sheria Mbalimbali Binafsi za Kiislamu).13-Wasifu mfupi wa Imam Ali bin Abi Talib (as). 14-Wasifu wa Imam Ali bin Mussa Al-Ridha (as). 15-Wasifu wa Imam Hassan al-Mujtaba – Imam wa Pili – (a.s). 16-Wasifu wa Imam Hussein bin Ali (as). 17-Wasifu wa Imam Muhammad bin Hassan al-Mahdi (atfs). 18-Wasifu wa Imam Mussa bin Jaafar (as).

Na vitabu vingine vingi vilivyoandikwa na Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi(ra) kwa Lugha ya Kiingereza pamoja na waandishi wengine ambavyo Dokta Mohammed Saleh Kanju alifanya kazi kubwa ya kiviweka katika Lugha ya Kiswahili ili kufikisha ilmu na maarifa ya Kiislamu yaliyomo ndanimwe kwa mamilioni ya watu wanaoongea Lugha Fasaha ya Kiswahili wa nchi za Afrika ya Mashariki na Nchi za Afrika ya Kati (zilizopo Katikati ya Bara la Afrika).

Mwenyezi Mungu Amrehemu Dokta Mohammed Saleh Kanju na Amfufue Kesho Siku ya Kiyama pamoja na Muhammad (saww) na Kizazi chake Kitukufu, Ahlul-Bayt wake (as).

🌐www.allamahrizvi.com

🏛️BonyadAkhtarTaban
🍃بنیاد اختر تابان

Related Articles

Leave a Reply

Check Also
Close
Back to top button
×